• HABARI MPYA

  Saturday, December 27, 2014

  THIERRY HENRY AIBUKIA KWENYE FILAMU

  MSHAMBULIAJI wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa, Thierry Henry atatokea kwenye sinema mwakani, 2015 baada ya kucheza fiamu ya Entourage.
  Nahodha huyo wa zamani wa Arsenal, Henry alitangaza kustaafu soka mapema mwezi huu katika klabu yaNew York Red Bulls ya Marekani.
  Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 37 amejiunga na kituo cha Televisheni cha Sky Sports kama mchambuzi na amethibitisha atasomea ukocha kwa matumaini ya kocha wa The Gunners, klabu aliyoichezea kwa miaka minane.
  Imposing: Henry was snapped by Doug Ellin in Beverly Hills with his dog
  Henry atacheza sehemu ndogo ya filamu ya Entourage ambayo itatolewa mwaka 2015

  Lakini nyota huyo wa zamani wa Ufaransa amecheza sehemu ndogo ya filamu ya kituo cha Televisheni Marekani, Entourage akiwa na nyota wa tasniya hiyo kama Ari Gold.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: THIERRY HENRY AIBUKIA KWENYE FILAMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top