• HABARI MPYA

  Wednesday, December 24, 2014

  ALEX SONG ATEMWA CAMEROON KIKOSI CHA AFCON, ETO’O NAYE…

  Na Mwandishi Wetu, YOUNDE
  KIUNGO wa kimataifa wa Cameroon, Alexandre Song ametemwa katika kikosi cha Simba Wasiofungika kwa ajili ya Fainali za Mataia ya Afrika mwakani.
  Habari hizo zinakuja saa kadhaa baada ya mchezaji huyo kuripotiwa kuiambia klabu yake, West Ham United nia yake ya kwenda kwenye fainali hizo nchini Equatorial Guinea.
  Tayari The Hammers watawakosa Wasenegal wawili, Diafra Sakho na Cheikhou Kouyate, ambao imethibitishwa watakwenda kwenye michuano hiyo mikubwa Afrika. 
  Kama na Song angeondoka angekuwa mchezaji wa tatu kwenye kikosi cha Sam Allardyce kwenda AFCON 2015.
  Alex Song kulia na Samue Eto'o kushoto wote hawatakuwemo kikosi cha Cameroon AFCON

  Shirikisho la Soka Cameroon (FECAFOOT), leo limeanza kutangaza kwa awamu kikosi cha timu ya taifa mjini Yaounde kupitia akaunti yake rasmi ya Twitter. 
  Song ameichezea West Ham mechi 11 kati ya 17 za Ligi Kuu ya England msimu huu, akipiga mipira 25 ya kupitia miguuni mwa wapinzani, kuzuia mitatu, lakini alikuwa ana mchango mkubwa kikosi cha Cameroon katika mechi za kufuzu AFCON.
  Kocha wa timu ya taifa, Volke Finke amepania kutengeneza kikosi bila kumshirikisha mshambuliaji mtata na gwiji, Samuel Eto’o aliyeichezea timu hiyo kwa miaka mingi na kwa mafanikio pia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ALEX SONG ATEMWA CAMEROON KIKOSI CHA AFCON, ETO’O NAYE… Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top