• HABARI MPYA

  Friday, December 26, 2014

  MAN CITY YAILAZA 3-1 WBA ENGLAND

  MABINGWA watetezi, Manchester City wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya West Bromwich Albion katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo Uwanja wa The Hawthorns.
  Mabao ya City leo yamefungwa na Fernando dakika ya nane, Yaya Toure kwa penalti dakika nane baadaye na David Silva dakika ya 34. 
  City inafikisha pointi 42 kwa ushindi huo na kuendelea kubaki nafasi ya pili, nyuma ya vinara Chelsea wenye pointi 45, baada ya timu zote kucheza mechi 18. Bao pekee la WBA limefungwa na Ideye dakika ya 86. 
  Kikosi cha West Brom kilikuwa; Foster, Wisdom, McAuley, Lescott, Pocognoli/Gamboa dk67, Morrison, Mulumbu, Sessegnon, Gardner/Brunt dk67, Varela/Ideye dk67 na Berahino.
  Manchester City: Hart, Sagna, Demichelis, Mangala, Clichy, Fernando, Toure/Fernandinho dk69, Jesus Navas, Silva/Kolarov dk63, Nasri/Lampard dk75 na Milner.
  Manchester City players Yaya Toure, David Silva, Jesus Navas, Samir Nasri, Fernando and Bacary Sagna celebrate their victory
  Wachezaji wa Manchester City, Yaya Toure, David Silva, Jesus Navas, Samir Nasri, Fernando na Bacary Sagna wakishangilia ushindi wao leo 
  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2887475/West-Brom-1-3-Manchester-City-Fernando-Yaya-Toure-David-Silva-strike-comfortable-victory-Baggies.html#ixzz3N1j2h9Ei
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY YAILAZA 3-1 WBA ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top