// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MAN CITY YAENDA 16 BORA LIGI YA MABINGWA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MAN CITY YAENDA 16 BORA LIGI YA MABINGWA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, December 11, 2014

    MAN CITY YAENDA 16 BORA LIGI YA MABINGWA

    MABAO ya Samir Nasri na Pablo Zabaleta yameipeleka Manchester City katika hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, kufuatia ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji AS Roma jana nchini Italia. Mfaransa Nasri alifunga dakika ya 60, kabla ya Zabaleta kufunga la pili dakika ya 86, ushindi ambao unaihakikishia City kumaliza katika nafasi ta pili kwenye Kundi E, nyuma ya Bayern Munich, ambao waliifunga CSKA Moscow 3-0 jana.
    Ushindi wa Bayern dhidi ya CSKA unamaanisha City hata kama wangetoa sare wangefuzu
    City ambao jana waliwakosa nyota wao Sergio Aguero, Vincent Kompany (wote majeruhi) na Yaya Toure anayetumikia adhabu, wana kila sababu ya kumshukuru kipa wao, Joe Hart kwa kazi nzuri hadi Mchezaji Bora wa Mechi.
    Kikosi cha Roma kilikuwa: De Sanctis, Maicon/Florenzi dk79, Manolas, Yanga-Mbiwa, Holebas, Ljajic/Iturbe dk67, Nainggolan, Keita, Gervinho, Pjanic na Totti/Destro dk70.
    Man City: Hart, Zabaleta, Demichelis, Mangala, Clichy, Jesus Navas/Silva dk67, Fernandinho, Fernando, Milner, Nasri/Kolarov dk88 na Dzeko/Jovetic dk78.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN CITY YAENDA 16 BORA LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top