• HABARI MPYA

  Wednesday, December 31, 2014

  TORRES AANZA KAZI ATLETICO MADRID, KUIVAA REAL JANUARI 7 KOMBE LA MFALME

  MSHAMBULIAJI Fernando Torres jana amefanya mazoezi kwa mara ya kwanza tangu arejee Atletico Madrid.
  Mpachika mabao huyo amnaye nyota yake imefifia kwa sasa, amekamilisha uhamisho wa mkopo kutoka AC Milan mapema wiki hii na anatarajiwa kucheza kwa mara ya kwanza dhidi ya Levante Jumamosi. 
  Awali, Mspanyola huyo alipata mapokezi mazuri wakati anawasili Uwanja wa Ndege wa Barajas mjini Madrid. 
  Fernando Torres trains at Atletico Madrid's sports grounds in Majadahonda, near Madrid for the first time since his return
  Fernando Torres akifanya mazoezi na Atletico Madrid mjini Majadahonda, jirani na Madrid kwa mara ya kwanza tangu arejee
  Torres also answered questions for the waiting press ahead of his famous return to the club where he made his name 
  Torres akijibu maswali ya Waandishi wa Habari baada ya kuwasili Madrid
  On Monday Torres tweeted his excitement to be back at the club where he became a star as a teenager
  Jumatatu, Torres alitweet juu ya namna alivyovutiwa kurejea katika klabu iliyomuibua akiwa kinda.
  Kwenye akaunti yao ya Instagram, Atletico Madrid wametangaza furaha yao juu ya kurejea kwa mshambuliaji huyo.
  Mabingwa hao wa La Liga wameandika: 'Fernando @Torres ametua Uwanja wa Ndege wa Barajas. Anawasalimia wote.'
  Torres, mwenye umri wa miaka 30, amekubali kujiunga tena na klabu yake ya utotoni kwa mkopo kutoka AC Milan Jumatatu na atakuwa huko hadi mwisho wa msimu wa 2015-2016.
  Alipokuwa katika klabu hiyo mara ya kwanza, mshindi huyo wa Kombe la Dunia alicheza mechi 214 Atletico na kufunga mabao 84. Mechi yake ya kwanza baada ya kurejea inatarajiwa kuwa dhidi ya wapinzani wao wa Jiji, Real kwenye 16 Bora ya Kombe la Mfalme Januari 7, mwakani ingawa mabingwa hao wa La Liga wanatarajiwa kucheza na Levante Januari 3. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TORRES AANZA KAZI ATLETICO MADRID, KUIVAA REAL JANUARI 7 KOMBE LA MFALME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top