• HABARI MPYA

  Sunday, December 28, 2014

  SIMBA SC SAFARI TANGA NA MGAMBO JKT, YANGA WAKIMALIZA NA AZAM WANA MBEYA CITY TAIFA

  Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
  WAKATI raundi ya nane ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inakamilika leo (Desemba 29 mwaka huu) kwa mechi tatu, ligi hiyo itaingia raundi ya tisa Januari 3 mwakani kwa mechi tano.
  Coastal Union itacheza na JKT Ruvu katika Uwanja wa Mkwakwani, Ruvu Shooting itaikaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Mabatini, Azam itakuwa mwenyeji wa Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Azam Complex, Stand United itakuwa mgeni wa Polisi Morogoro kwenye Uwanja wa Jamhuri wakati Mbeya City na Yanga zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Sokoine.
  Kocha wa Simba SC, Patrick Phiri atasafiri na timu yake Tanga wiki ijayo

  Ligi hiyo ambayo itachezwa mfululizo (non-stop) hadi itakapomalizika Mei 9 mwakani, itakamilisha raundi ya tisa Januari 4 mwakani kwa mechi kati ya Mgambo Shooting na Simba kwenye Uwanja wa Mkwakwani, na Tanzania Prisons itakayokuwa mwenyeji wa Ndanda kwenye Uwanja wa Sokoine.
  Nayo mechi kati ya Mtibwa Sugar na Stand United ambayo jana ilivunjwa na mvua dakika ya 6 imemaliziwa leo ambapo timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1.
  Wakati huo huo, mechi ya ligi iliyochezwa jana usiku kwenye Uwanja wa Azam Complex imemalizika kwa wageni Ruvu Shooting kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Ruvu. Bao hilo lilifungwa kipindi cha kwanza kwa mkwaju wa penalti uliopigwa na Hamisi Kasanga.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC SAFARI TANGA NA MGAMBO JKT, YANGA WAKIMALIZA NA AZAM WANA MBEYA CITY TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top