• HABARI MPYA

  Saturday, December 27, 2014

  MVUA YAVUNJA MECHI YA MTIBWA NA STAND, COASTAL UNION SARE NA PRISONS MBEYA

  Na Mwandishi Wetu, MBEYA
  COASTAL Union imelazimisha sare ya bila kufungana na wenyeji Prisons Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya jioni ya leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Matokeo hayo, yanaifanya Coastal itemize pointi 12 baada ya kucheza mechi nane, wakati Prisons nayo inatimiza pointi saba baada ya mechi nane pia.
  Mchezo mwingine wa Ligi Kuu leo, kati ya vinara Mtibwa Sugar na Stand United Uwanja wa Manungu, Morogoro umevunjika dakika ya sita kutokana na mvua kubwa kunyesha.
  Wachezaji wa Coastal Union leo wametoa sare ugenini

  TFF imeamua sasa mchezo huo utamaliziwa kesho. Mechi nyingine ya Ligi Kuu kati ya JKT Ruvu na Ruvu Shooting inachezwa usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Hadi Ligi Kuu inasimama baada ya raundi ya saba, Mtibwa Sugar walikuwa kileleni kwa pointi zao 15, wakifuatiwa na Azam FC na Yanga SC zilizofungana kwa pointi 13 kila moja na hata wastani wa mabao ukiwa sawa. Yanga SC na Azam zitamenyana kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MVUA YAVUNJA MECHI YA MTIBWA NA STAND, COASTAL UNION SARE NA PRISONS MBEYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top