• HABARI MPYA

  Sunday, December 21, 2014

  COASTAL WACHEZA NA KOMBAINI YA MOMBASA LEO

  Na Mwandishi Wetu, TANGA.
  TIMU ya Coastal Union ‘Wagosi wa Kaya’ leo inatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki na Kombaini ya Mombasa, nchini Kenya ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara.
  Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Manispaa ya Mombasa ambao unaatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kutokana na joto lililopo mjini Mombasa kuelekea mechi hiyo.
  Akizungumza jana, Ofisa Habari wa Coastal Union, Oscar Assenga amesema maandalizi ya mechi hiyo yamekamilika kwa asilimia kubwa na kinachosubiriwa ni siku ya mechi hiyo ambayo ni leo.

  Assenga amesema kuwa mechi hiyo itakuwa ni kipimo tosha kwa kocha mpya wa timu hiyo, James Nandwa kuangalia kiwango cha timu hiyo kabla ya kuwavaa wapinzani wao Prisons katika Ligi Kuu.
  Hata hiyo, amesema kuwa  licha ya kocha huyo kuangalia kiwango cha wachezaji ambapo mechi hiyo itakuwa ni ya pili kusimama kwenye bechi ya kwanza ilikuwa ni kati ya Coastal Union dhidi ya Mwadui ya shinyanga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: COASTAL WACHEZA NA KOMBAINI YA MOMBASA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top