• HABARI MPYA

  Friday, December 26, 2014

  ROONEY APIGA MBILI, AMSETIA VAN PERSIE MAN UNITED IKISHINDA 3-1

  MANCHESTER United imeendelea kufanya vizuri katika Ligi Kuu ya England kufuatia ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Newcastle Uwanja wa Old Trafford.
  Ilikuwa ni siku nzuri kwa Nahodha Wayne Rooney, aliyeifungia Manchester United mabao mawili na kutoa pasi ya bao moja, la tatu.
  Rooney alifunga bao la kwanza kwa pasi ya Radamel Falcao dakika ya 23 katika shambulizi alilolianzisha mwenyewe kutokea nyuma, kabla ya kufunga la pili dakika 13 baadaye kwa pasi la Juan Mata.
  Nahodha huyo wa England pia, akampasia mpira mzuri Robin van Persie kufunga bao la tatu kwa kichwa dakika ya 53, kabla ya Papis Cisse kuifungia bao la kufutia machozi Newcastle kwa penalti dakika ya 87. 
  Kwa ushindi huo, Mashetani Wekundu wanaendelea kukamata nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu, wakizidiwa pointi 10 na vinara, Chelsea
  Kikosi cha Manchester United kilikuwa; De Gea, Jones, McNair, Evans, Valencia/Rafael dk80, Rooney, Carrick/Fletcher dk62, Young, Mata, Falcao/Wilson dk65 na Van Persie. 
  Newcastle: Alnwick, Janmaat, Steven Taylor, Coloccini, Dummett/Cabella dk63, Anita, Colback, Armstrong/Cisse dk63, Sissoko, Gouffran na Perez/Vuckic dk82.
  Rooney runs away with his arms outstretched after scoring for the home side against Newcastle in the 36th minute 
  Rooney akikimbia kushangilia baada ya kuifungia United dhidi ya Newcastle leo 

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2887471/Manchester-United-3-1-Newcastle-United-Wayne-Rooney-double-Robin-van-Persie-strike-sees-Louis-van-Gaal-s-claim-win.html#ixzz3N1dX3fSW 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ROONEY APIGA MBILI, AMSETIA VAN PERSIE MAN UNITED IKISHINDA 3-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top