• HABARI MPYA

  Tuesday, December 23, 2014

  CHELSEA YAJITANUA KILELENI LIGI KUU ENGLAND

  CHELSEA imejitanua kileleni mwa Ligi Kuu ya England kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji Stoke City Uwanja wa Britania usiku huu.
  The Blues ya kocha Mreno, Jose Mourinho sasa inatimiza pointi 42 baada ya mechi 17, ikiwazidi kwa pointi tatu, mabingwa watetezi, Manchester City waliocheza mechi 17 pia. Man United wenye pointi 32 ni wa tatu baada ya kucheza mechi 17 pia.
  John Terry aliifungia bao la kwanza Chelsea akimalizia mpira wa kona uliopigwa na kiungo Cesc Fabregas. Phil Bardsley alikuwa mwenye bahati kwa kuonyeshwa kadi ya njano tu baada ya kumchezea rafu mbaya Eden Hazard.
  Fabregas akaifungia bao la pili Chelsea zikiwa zimebakia dakika 12 kupulizwa kipyenga cha mwisho na kuwaweka sawa Th Blues kileleni.
  Kikosi cha Stoke City kilikuwa; Begovic, Bardsley, Shawcross, Muniesa, Pieters, Nzonzi, Cameron/Adam dk68, Walters, Bojan, Arnautovic/Assaidi dk82 na Crouch/Diouf dk63.
  Chelsea; Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Mikel, Matic, Willian/Schurrle dk80, Fabregas, Hazard/Zouma dk90 na Costa/Drogba dk85.
  Cesc Fabregas slides on his knees to celebrate after his goal secured the win for Chelsea, who will be top on Christmas Day
  Cesc Fabregas akiwa amepiga magoti kushangilia baada ya kuifungia bao la pili Chelsea
  Hazard is sent flying by the force of the challenge from former Sunderland and Manchester United defender
  Beki wa Stoke, Phil Bardsley akimchezea rafu Edin Hazard wa Chelsea 

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2884124/Stoke-0-2-Chelsea-John-Terry-rises-occasion-Cesc-Fabregas-seals-win-Blues-secure-spot-Christmas.html#ixzz3MgF7AXbv Christmas.html#ixzz3MgEnLMfw
  Follow us: @MailOnline on Twitter | DailyMail on Facebook
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA YAJITANUA KILELENI LIGI KUU ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top