• HABARI MPYA

    Tuesday, June 30, 2026

    PARAGUAY YAITUPA NJE UJERUMANI KWA MATUTA KOMBE LA DUNIA


    TIMU ya Paraguay imefanikiwa kwenda Hatua ya 16 Bora Fainali za Kombe la Dunia baada ya ushindi wa penalti 4-3 kufuatia sare ya 1-1 na Ujerumani usiku wa jana Uwanja wa Gillette mjini Foxborough, Norfolk County, Massachusetts, Marekani.
    Kiungo mshambuliaji wa RC Strasbourg ya Ufaransa, Julio Cesar Enciso Espínola alianza kuifungia Paraguay dakika ya 42, kabla ya mshambuliaji Kai Lukas Havertz wa mabingwa wa England, Arsenal kuisawazishia Ujerumani dakika ya 54.
    Kwenye mikwaju ya penalti walioifungia Paraguay ni Maurício, G. Gómez, Galarza na Canale huku Sanabria na Balbuena pekee wakikosa, wakati kwa upande wa Ujerumani waliofunga ni Kimmich, Musiala na Amiri huku Havertz, Woltemade na Tah wakikosa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PARAGUAY YAITUPA NJE UJERUMANI KWA MATUTA KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top