• HABARI MPYA

  Wednesday, December 31, 2014

  CHELSEA KUMUUZA UJERUMANI HAZARD PAUNI MILIONI 6.3

  KLABU ya Borrusia Monchengladbach imetoa ofa ya Pauni Milioni 6.3 kwa ajili ya kumnunua winga wa Chelsea, Thorgan Hazard.
  Kinda huyo wa umri wa miaka 21, mdogo wa Eden amekuwa kivutio akicheza kwa mkopo katika klabu hiyo ya Ujerumani, ambayo sasa inataka kumbeba jumla.
  Mazungumzo yanaendelea baina ya pande hizo mbili tangu wiki iliyopita na klabu hiyo inayoshika nafasi ya nne katika msimamo wa Bundesliga wanataka kuimarisha kikosi chao katika kuwania kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.
  Thorgan Hazard (centre) is enjoying a successful loan spell at German club Borussia Monchengladbach
  Thorgan Hazard (katikati) anafurahia mafanikio na  Borussia Monchengladbach Ujerumani

  Hazard mdogo pia amewahi kucheza kwa mkopo Zulte Waregem ya Ubelgiji na anaamini akiondoka moja kwa moja Stamford Bridge atakuwa na mwanzo mwingine katika maisha yake ya soka.
  Kinda huyo wa zamani wa Lens amecheza mechi 15 Bundesliga msimu huu na kufunga bao moja, huku akitoa pasi za nne za mabao.
  Hazard alijiunga na Chelsea kwa dau dogo tu kutoka klabu hiyo ya Ufaransa Julai 2012, mwezi mmoja baada ya kaka yake, Eden kusajiliwa kutoka Lille kwa Pauni Milioni 32. 
  Hazard mdogo ameichezea mara moja timu yake ya taifa, Ubelgiji mwaka 2013 na alikuwa kwenye orodha ya wachezaji wa akiba kwa ajili ya Kombe la Dunia mwaka huu.
  Eden Hazard (left), pictured in action against Southampton, has been a huge hit since joining Chelsea in 2012
  Eden Hazard (kushoto) akiicheza dhidi ya Southampton, amekuwa na mafanikio tangu ametua Chelsea mwaka 2012
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA KUMUUZA UJERUMANI HAZARD PAUNI MILIONI 6.3 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top