• HABARI MPYA

  Tuesday, December 30, 2014

  TEARGAS’ AREJEA GOR MAHIA; SABA WATEMWA

  Na Vincent Malouda, NAIROBI
  ALIYEKUWA kiungo wa Gor Mahia Victor Ali Hassan Abondo maarufu kama ‘Teargas’ (pichani kushoto) miongoni mwa mashabiki wa klabu hicho yumo mbioni kurejea tena kwenye timu hiyo.
  Gor Mahia inasemekana imewaomba Tusker imwachilie kiungo huyo ili wamsajili huku wakiharakisha kuwasilisha kikosi chao kwenye makao makuu ya CAF, Misri kwa ajili ya mechi za klabu bingwa mwaka ujao.
  “Wametuomba tumwachilie Abondo ajiunge nao nasi tumekubali. Tutamaliza maswala mengine ya uhamisho juma lijalo japo kwa sasa wapo huru kumsajili,” afisa mkuu mtendaji wa Tusker FC Charles Obiny aliliambia BIN ZUBEIRY.
  Abondo ambaye ana mkataba mmoja na Tusker alitemwa Gor Mahia Juni 2013 na kujiunga na wanavileo hao na sasa anarejea tena klabuni humo.
  Gor wamekuwa wepesi wa kurejesha vifaa vyao vya awali kwa mfano wa Collins ‘Gatuso’ Okoth, Rama Salim, George ‘Blackberry’ Odhiambo na wengineo waliyorejea kwa wakati mmoja K’Ogalo.
  Abondo ameonekana katika afisi za Gor leo Jumanne kumalizia maswala binafsi.
  Gor tayari imewanasa Dirkir Glay, Martin Werunga (mabeki), David Magoma (kiungo), Earnest Wendo, Ronald Omino na Zachary Taofiq (mastraika) na kuwachilia wasabi; Patrick Oboya, Angelo Okumu, Simon Mburu, Kennedy Ayong, mganda Charles Bruno, Innocent Mutiso na Ian Niva.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TEARGAS’ AREJEA GOR MAHIA; SABA WATEMWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top