• HABARI MPYA

  Sunday, December 21, 2014

  MALINZI MKUBWA AULA TENA BMT

  DIONIZ Malinzi ameteuliwa tena kwa mara ya pili mfululizo kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT).
  Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara, ametaja Baraza jipya la Michezo na Malinzi, kaka wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ataendelea kuwa Mwenyekiti. 
  Dioniz Malinzi (kushoto) ameula tena BMT

  Waziri pia amewateua Jamal Rwambow, Alex Mgongolwa, Jenniffer Mmasi Shang’a na Zainab Mbiro kuendelea kuwa Wajumbe wa BMT.
  Wajumbe wapya ni Zacharia Hans Poppe, Mohamed Bawaziri, Zainab Vullu, Mbunge wa Viti Maalum, Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, Cresscentius Magori wa NSSF na John Ndumbaro. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MALINZI MKUBWA AULA TENA BMT Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top