// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); NYOTA WA TIMU YA TAIFA BRAZIL APATA AJALI YA GARI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE NYOTA WA TIMU YA TAIFA BRAZIL APATA AJALI YA GARI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, December 08, 2014

    NYOTA WA TIMU YA TAIFA BRAZIL APATA AJALI YA GARI

    MWANASOKA bora wa kike wa dunia mara tano, Marta amepata ajali ya gari nchini Brazil.
    Nyota huyo wa timu ya taifa ya wanawake wa Brazil alipelekwa hospitali kwa vipimo, lakini ikagundulika hajapata madhara makubwa na akaruhusiwa baada tu ya ajali hiyo Jumamosi.
    Tukio hilo lilitokea Kaskazini Mashariki mwa Brazil, ambako nyota huyo alikwenda kwa ajili ya mapumziko. Mamlaka zimesema kwamba Marta alipoteza mwelekeo wakati anaendesha gari lake aina ya Audi na kulipeleka pembezoni mwa barabara.
    Brazilian superstar Marta escaped with only bruises after crashing her car on holiday 
    Nyota wa Brazili, Marta amepata ajali akiwa mapumzikoni 

    Tovuti ya GloboEsporte imeandika kwamba watu wengine watatu waliokuwamo kwenye gari hilo hawakuumia sana pia.
    Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28 ameripotiwa kwamba alikuwa anarejea kutoka nyumbani kwa rafiki yake wakati ajali hiyo inatokea mchana katika mji wa Santana do Ipanema.
    Marta ataichezea Brazil katika mashindano ya kimataifa mji Mkuu wa nchi hiyo, Brasilia wiki hii.
    The five time world player of the year is expected to play for the Brazil women's team next week
    Mwanasoka Bora wa Dunia mara tano anatarajiwa kuichezea timu ya taifa ya wanawake ya Brazil wiki hii
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NYOTA WA TIMU YA TAIFA BRAZIL APATA AJALI YA GARI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top