TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
Mabao ya Azam FC yamefungwa na beki Muivory Coast, Landry Ahoutou Angenor Zouzou dakika ya pili na kiungo mzawa, Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ dakika ya 32 hilo likiwa bao lake la 15 la msimu na kuendelea kuongoza mbio za ufungaji Bora.
Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 61, ingawa inabaki nafasi ya pili, wakati Coastal Union inabaki na pointi zake 33 nafasi ya tisa kufuatia timu hizo nazo kucheza mechi 29 pia.



.png)
0 comments:
Post a Comment