VIGOGO Simba SC, wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida Black Stars katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Meja Jenerali Charles Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.
Mabao ya Simba SC yamefungwa na mawinga, Elie Mpanzu Kibisawala kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (drc) dakika ya 28 na Alain Anicet Oura kutoka Ivory Coast dakika ya 59.
Kwa ushindi huo, Simba SC wanafikisha pointi 70, ingawa wanabaki nafasi ya pili wakizidiwa pointi mbili na mabingwa watetezi, Yanga SC kufuatia timu zote kucheza mechi 29 kuelekea mechi za mwisho za msimu Jumanne.
Kwa upande wao Singida Black Stars baada ya kupoteza mchezo huo wanabaki na pointi zao 50 kufuatia kucheza mechi 29 pia wakisalia pia katika nafasi ya nne.



.png)
0 comments:
Post a Comment