// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); CHELSEA YATAKATA KAMA KAWA ULAYA, YATINGA MTOANO LIGI YA MABINGWA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE CHELSEA YATAKATA KAMA KAWA ULAYA, YATINGA MTOANO LIGI YA MABINGWA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, December 11, 2014

    CHELSEA YATAKATA KAMA KAWA ULAYA, YATINGA MTOANO LIGI YA MABINGWA

    CHELSEA imefuzu hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya kufuatia ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Sporting Lisbon Uwanja wa Stamford Bridge usiku wa jana.  
    The Blues sasa inaungana na Schalke kufuzu hatua hiyo kutoka Kundi G baada ya timu zote kushinda jana.
    Kocha Mreno, Jose Mourinho aliwapumzisha wachezaji wake kadhaa nyota, lakini Chelsea iling’ara kutokana na mabaoya Cesc Fabregas kwa penalti dakika ya nane baada ya Filipe Luis kuchezewa rafu kwenye boksi, Andre Schurrle aliyefunga la pili dakika ya 16 na John Mikel Obi la tatu dakika ya 56.
    Jonathan Silva ndiye aliyeifungi bao la kufutia machozi Sporting Lisbon dakika ya 50.
    Kikosi cha Chelsea kilikuwa; Cech, Azpilicueta, Zouma, Cahill, Filipe Luis, Mikel, Matic, Schurrle/Ramires dk74, Fabregas/Loftus-Cheek dk83, Salah/Remy dk71 na Diego Costa.

    Sporting Lisbon; Rui Patricio, Ricardo Esgaio, Mauricio, Paulo Oliveira, Silva, Adrien Silva, William Carvalho/Montero, Jaoi Mario/Andre Martins, Carillo, Slimani, Capel/Carlos Mane dk61.
    The former Arsenal midfielder salutes to the crowd after giving the Blues the lead on Wednesday night
    The former Arsenal midfielder salutes to the crowd after giving the Blues the lead on Wednesday night

    PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2869079/Chelsea-3-1-Sporting-Lisbon-Cesc-Fabregas-Andre-Schurrle-John-Obi-Mikel-target-Champions-League.html#ixzz3LYeXABci 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHELSEA YATAKATA KAMA KAWA ULAYA, YATINGA MTOANO LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top