• HABARI MPYA

  Wednesday, December 10, 2014

  DK SHEIN MGENI RASMI TUZO ZA WANAMICHEZO BORA

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  RAIS wa Zanzibar, Dk Ali Mohame ndiye mgeni rasmi katika Tuzo za Wanamichezo Bora za Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), hafla itakayofanyika usiku wa Ijumaa katika ukumbi wa VIP Diamond Jubilee, Dar es Salaam.
  Makamu Mwenyekiti wa TASWA, Egbert Mkoko amesema asubuhi ya leo katika Mkutano na Waandishi wa Habari ukumbi wa City Sports Lounge, Dar es Salaam kwamba wanaishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwasaidia kumpata Dk Shein kuwa mgeni rasmi katika shughuli hiyo.
  Mkoko amesema maandalizi yote kwa ujumla yamekamilika kuelekea shughuli hiyo na amewataka wanamichezo wote walioalikwa kuzingatia muda wa kufika kwa mujibu wa kadi zao za mialiko, ili zoezi liende na kumalizika kwa wakati.
  Amesema wana imani kubwa kwamba tuzo hizo zitakuwa na mvuto na kuwashukuru wadhamini wao kwa kufanikisha tuzo hizo.
  Katika tuzo za mwaka huu, beki na Nahodha wa Yanga SC, Nadir Haroub Ali ‘Cannavaro’ amepambanishwa na mshambuliaji wa Simba SC, Elias Maguli na kiungo wa Azam FC, Erasto Edward Nyoni katika kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Tanzania mwaka 2013/2014.
  Makamu Mwenyekiti wa TASWA, Egbert Mkoko (katikati) akionyesha tuzo za washindi sawa na Katibu, Amir Mhando kulia. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Mwani Nyangassa

  Tuzo ya Mwanasoka wa kigeni anayecheza Tanzania inawaniwa na Kipre Tchetche wa Azam FC, Amisi Tambwe wa Simba SC  na Mbuyu Twite wa Yanga SC.
  Tuzo ya Watanzania wanaocheza nje inawaniwa na Richard Laizer Muendesha Baiskeli Afrika Kusini na Uswisi, Mbwana Sammata na Thomas Ulimwengu, wote wa TP Mazembe ya DRC.
  Ngumi za Kulipwa wanachuana Francis Cheka, Ramadhani Shauri na Said Mbelwa, Olimpiki Maalum, Raphael Kalukula, Pazi Mwinyimkuu na Hatibu Matali, Wanawake: Blandina Blasi, Shida Jaha na Mwanaharusi Risasi.
  Mpira wa Kikapu kwa wanaume; Lusajo Samwel (Oilers), Erick Mchemba (ABC), wanawake: Sajda Ahmed Lyamaiga (Don Bosco Lioness), Rehema Silomba (Don Bosco Lioness) na Orlyn Titus (Don Bosco Lioness).
  Mpira wa Magongo wanaume ni Yohana Wilson, Focus Paul, Deep Vaja, Wanawake: Valentina Quarantta, Kidawa Seremala na Mary Mhina, Mpira wa Wavu; Wanawake: Yasinta Remmy (Jeshi Stars), Hellena Richard (Magereza) na Teddy  Abwao (Jeshi Stars), wanaume ni Kelvin Peter Severino (Magereza), Nassoro Sharifu (Jeshi Stars) na Athuman Rupia (Jeshi Stars).
  Katika Riadha, wanawake ni Zakia Mrisho, Jaqueline Sakilu na Catherine Lange, Wanaume ni Alphonce Felix, Dickson Marwa na Fabian Nelson.
  Baiskeli ni Salome Donald, Martha Anthon na Sophia Adson upande wa wanawake, wakati wanaume ni Richard Laizer, Hamisi Mskala na Gerald Konda, Gofu wanaume ni Nuru Mollel, Abasi Adam na Frank Mwinuka, wakati wanawake ni Madina Iddi, Hawa Wanyeche na Angel Eaton, Gofu ya Kulipwa ni Hassan Kadio, Yassin Salehe na Geoffrey Leverian.
  Upande wa Judo wanaume ni Kombo Masoud Amour na Mbarouk Suleiman wakati wanawake ni Grace Alfonce Mhanga na Salma Omari Othman, Tenisi Walemavu wanaume ni Novatus Emmanuel Temba, Yohana  Assa Mwila na Juma Mohamed Hamisi, wakati  wanawake ni Rehema Selemani Saidi na Bihawa Mustafa Ituji. 
  Tenisi wanaume ni Tumaini Martin, Emmanuel Malya na Omari Sulle, wanawake: Rehema Athumani, Edna John na Georgina Kaindoh, Netiboli, Doritha Mbunda (JKT Mbweni), Berina Kazinja (Magereza Moro) na Andressa Andrea (Magereza Moro),
  Katika Ngumi za Ridhaa ni Fabian Gaudence, Ahmed Furahisha na Ally Abdul Ahmed, Mmpira wa Mikono wanaume ni Hemedi Salehe (JKT), Msafiri Makoti (Ngome) na Abinery Kusena (JKT), wakati wanawake ni Veronica Mapunda, Subira Omary na Mwajabu Lugato
  Kwa upande wa Wanamichezo Chipukizi ni Omari Sulle (Tenisi), Sheridah Boniface (Soka wanawake) na Aishi Manula (Soka wanaume-Azam), wakati pia kutakuwa na Tuzo ya Heshima ambayo itatangazwa ukumbini siku ya kilele cha tafrija Desemba 12, mwaka huu. Aidha, Nyaulawa amesema kwamba Kriketi, mpira wa meza, Kareti, Paralimpiki majina yatatangazwa kabla ya Ijumaa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DK SHEIN MGENI RASMI TUZO ZA WANAMICHEZO BORA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top