• HABARI MPYA

    Thursday, July 16, 2026

    AZAM FC YASAJILI BEKI MBELGIJI ALIKUWA ANACHEZA AFRIKA KUSINI


    KLABU ya Azam FC imemtambulisha beki wa kati Mbelgiji, Henri Braham Stanic kuwa mchezaji wake mpya kuelekea msimu ujao, akijiunga na timu hiyo kutoka Stellenbosch FC ya Afrika Kusini.
    Stanic anaondoka Stellenbosch FC baada ya msimu mmoja tu tangu awasili Julai 15 mwaka jana, 2025 akitokea Balzan FC ya Malta baada ya awali kucheza Liepaja ya Latvia, Jerv ya Norway, OH Leuven U23, Anderlecht U18, OH Leuven U21 kufuatia kupikwa katia akadmi ya Anderlecht, zote za Ubelgiji.
    Henri Braham Stanic alizaliwa nchini Ubelgiji, mama yake akitokea Kongo na baba yake akitokea Togo na wazazi wake walikutana awali katika kituo cha Wakimbizi Ubelgiji walipokuwa wakitafuta hifadhi. 
    Kwa sababu hawakuwa na hati za kisheria wakati wa kuzaliwa kwake, wakili wa Ubelgiji anayeitwa Vladimir Stanic alijisajili kama baba yake halali ili kumsajili chini ya sheria za Ubelgiji, ambapo ndipo jina lake la mwisho linapoanzia.
    Anakuwa mchezaji mpya wa pili baada ya winga Muivory Coast, Kipré Tiagori Emmanuel Junior Zunon ‘Kipre Junior’ aliyetambulishwa jana kujiunga tena na Azam FC akitokea MC Algiers ya Algeria. 
    Kipre Junior anarejea Azam FC ambako awali alicheza kuanzia msimu wa 2022-2023 akitokea SOL FC d’Abobo ya kwao, Ivory Coast hadi 2024-2025 alipohamia MC Algiers.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YASAJILI BEKI MBELGIJI ALIKUWA ANACHEZA AFRIKA KUSINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top