• HABARI MPYA

  Sunday, May 09, 2021

  TFF YAWAOMBA RADHI MASHABIKI NA WADAU KWA KUAHIRISHWA KWA MECHI YA SIMBA NA YANGA JANA MKAPA

  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeomba radhi kwa wadau wa soka baada ya kutoufanyika kwa mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baina ya watani wa jadi, Simba na Yanga uliopangwa kufanyika jana Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kufuatia kutokea mkanganyiko wa muda.
  Taarifa ya TFF asubuhi ya leo imesema kwamba wametoa maelekezo kwa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kutoa taarifa ya kina kuhusu kuahirishwa kwa mchezo huo pamoja na kushughulikia hatima ya wapenzi wa soka waliolipa viingilio kuingia Uwanjani.
  Jana Saa 8:33 mchana TFF lilitoa taarifa ya kusogeza mbele mechi kutoka Saa 11:00 jioni hadi Saa 1:00 usiku, ikisema imepokea agizo la Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kufanya hivyo, japo haikutaja sababu.

  Nusu saa baadaye Yanga SC wakatoa taarifa ya kupinga mabadiliko hayo wakisema yanakiuka kanuni inayotaka mchezo ubadilishwe muda sio chini ya Saa 24 kabla.
  Yanga SC waliwasili Uwanja wa Mkapa Saa 9:30 na kufanya mazoezi ya kuamsha misuli kabla ya kurejea vyumbani kusubiri muda wa kuitwa na waamuzi kuingia uwanjani, lakini Saa 11:30 wakaondoka kurejea kambini kwao.
  Baadaye Simba SC nao wakaingia uwanjani kufanya mazoezi pia kabla ya kurejea vyumbani na kisha nao kuondoka pia baada ya Saa ya Saa 1:15 usiku.
  Maelfu ya mashabiki waliobaki uwanjani walianzisha vurugu kudai warejeshewe viingilio, kabla ya Polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya.
  Huo ulikuwa mchezo huo marudiano wa msimu baada ya miamba hiyo kutoka sare ya 1-1 kwenye mechi ya kwanza Novemba 7, mwaka jana.
  Mechi ya kwanza hapo hapo Benjamin Mkapa, Yanga SC walitangulia kwa bao la penalti la mshambuliaji Mghana, Michael Sarpong kipindi cha kwanza, kabla ya beki Mkenya, Joash Onyango kuisawazishia Simba mwishoni kipindi cha pili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TFF YAWAOMBA RADHI MASHABIKI NA WADAU KWA KUAHIRISHWA KWA MECHI YA SIMBA NA YANGA JANA MKAPA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top