• HABARI MPYA

  Wednesday, May 05, 2021

  HARUNA MOSHI 'BOBAN' NA WENGINE 46 WASHIRIKI KOZI YA FIFA YA UFUNDISHAJI WA SOKA KWA VIJANA KARUME

  KIUNGO wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Haruna Moshi Shaaban 'Boban' ni miongoni mwa makocha wanaohudhuria Kozi ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) ya ufundishaji soka kwa vijana, maarufu kama Grassroots inayoendelea makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Uwanja wa Karume, Ilala Jijini Dar es Salaam. 
  Pamoja na Boban, mchezaji wa zamani wa Moro United, Simba, Coastal Union, Mbeya City na Yanga jumla ya washiriki 47 wanahudhuria Kozi hiyo ya mafunzo kwa vitendo ya siku tano inayoendeshwa Mkufunzi wa FIFA, Raymond Gweba.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HARUNA MOSHI 'BOBAN' NA WENGINE 46 WASHIRIKI KOZI YA FIFA YA UFUNDISHAJI WA SOKA KWA VIJANA KARUME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top