• HABARI MPYA

  Wednesday, May 19, 2021

  YACOUBA SOGNE NA TUISILA KISINDA WAFUNGA JAMHURI YANGA SC YAWACHAPA JKT TANZANIA 2-0 DODOMA

   VIGOGO, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma jioni ya leo.
  Mabao ya Yanga SC leo yanefungwa na mshambuliaji Mburkinabe, Yacouba Sogne dakika ya 27 na winga Mkongo, Tuisila Kisinda dakika ya 30.
  Kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 61 baada ya kucheza mechi 29, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa wastani wa mabao tu na mabingwa watetezi, Simba SC ambao pia wana mechi nne kiganjani, wakati JKT Tanzania inabaki na pointi zake 33 za mechi 30 katika nafasi ya 14.


  Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, wenyeji Gwambina FC wamelazimishwa sare ya 0-0 na Namungo FC Uwanja wa Gwambina, Misungwi mkoani Mwanza.
  Gwambina wanafikisha pointi 31 baada ya kucheza mechi 29 na kusogea nafasi ya 16 wakiizidi wastani wa mabao tu Ihefu SC, wakati Namungo imefikisha pointi 37 baada ya kucheza mechi 27, japo inabaki nafasi ya 10.
  Ikumbukwe mwishoni mwa msimu timu nne kati ya 18 zinazoshiriki Ligi Kuu zitashuka moja kwa moja na mbili zitakwenda kucheza na timu za Daraja la Kwanza kuwania kubaki kwenye ligi hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YACOUBA SOGNE NA TUISILA KISINDA WAFUNGA JAMHURI YANGA SC YAWACHAPA JKT TANZANIA 2-0 DODOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top