• HABARI MPYA

  Thursday, May 13, 2021

  SIMBA QUEENS NA YANGA PRINCESS KILA TIMU YATOA WACHEZAJI SITA KATIKA KIKOSI CHA TWIGA STARS

   WATANI wa jadi, Simba Queens na Yanga Princess kila timu imetoa wachezaji sita katika kikosi cha timu ya taifa ya wanawake Tanzania, Twiga Stars.
  Jumla ya wachezaji 27 wameitwa katika kikosi cha awali cha Twiga Stars kitakachoingia Kambini Mei 17, 2021 kujiandaa na mechi za kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
  JKT Queens na Ruvuma Queens ni timu nyingine zilizotoa wachezaji sita, wakati Mlandizi Queens na Fountain Gate zimetoa mchezaji mmoja mmoja huku Mwanahamisi Omar ya 'Gaucho' wa C.A.K. ya Morocco ni mchezaji pekee anayecheza nje aliyeitwa.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA QUEENS NA YANGA PRINCESS KILA TIMU YATOA WACHEZAJI SITA KATIKA KIKOSI CHA TWIGA STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top