• HABARI MPYA

    Friday, May 28, 2021

    DILUNGA WA SIMBA SC AENGULIWA KIKOSI CHA TAIFA STARS NAFASI YAKE APEWA MUDATHIR YAHYA WA AZAM FC

    KIUNGO wa Simba SC, Hassan Dilunga ameenguliwa kwenye kikosi kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kilichotajwa leo na kocha Mdenmark, Kim Poulsen na nafasi yake amepewa nyota wa Azam FC, Mudathir Yahya.
    Sasa Mudathir ataungana na wenzake watakaoingia kambini Juni 5, mwaka huu kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Malawi.
    Sasa kikosi hicho kinabaki na wachezaji saba wa klabu bingwa ya nchi, Simba SC, na wanne kutoka kila timu, Yanga SC na Azam FC zinazofuatia kwa ubora katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara.


    Wengine wanne wanacheza nje ya nchi, wawili hapa hapa Afrika na wawili Ulaya, wakati waliosalia wanatoka klabu mbalimbali za hapa nchini. timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kitakachoingia kambini Juni 5, mwaka huu kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Malawi.
    Katika kikosi hicho kuna wachezaji wanane kutoka klabu bingwa ya nchi, Simba SC, na wanne kutoka kila timu, Yanga SC na Azam FC zinazofuatia kwa ubora katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
    Wengine wanne wanacheza nje ya nchi, wawili hapa hapa Afrika na wawili Ulaya, wakati waliosalia wanatoka klabu mbalimbali za hapa nchini.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DILUNGA WA SIMBA SC AENGULIWA KIKOSI CHA TAIFA STARS NAFASI YAKE APEWA MUDATHIR YAHYA WA AZAM FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top