• HABARI MPYA

  Monday, May 03, 2021

  MESSI APIGA MBILI BARCELONA YAICHAPA VALENCIA 3-2 MESTALLA

  MUARGENTINA Lionel Messi jana amefunga mabao mawili, Barcelona ikiwachapa wenyeji, Valencia 3-2 katika mchezo wa La Liga Uwanja wa Mestalla.
  Messi alifunga dakika za 57 na 69, wakati bao lingine la Barca lilifungwa na Antoine Griezmann dakika ya 63 na ya Valencia yamefungwa na Carlos Soler dakika ya 83 na Gabriel Paulista dakika ya 50.
  Kwa ushindi huo, Barcelona inafikisha pointi 74 sawa na Real Madrid, baada ya wote kucheza mechi 34, ingawa inabaki nafasi ya tatu nyuma ya timu za Madrid, Atletico wakiongoza kwa pointi kwa pointi zao76 za mechi 34 pia.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MESSI APIGA MBILI BARCELONA YAICHAPA VALENCIA 3-2 MESTALLA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top