• HABARI MPYA

  Sunday, May 16, 2021

  COASTAL UNION WAJIWEKA PAGUMU BAADA YA KUCHAPWA MECHI YA TATU MFULULIZO LIGI KUU, TENA MKWAKWANI

   WENYEJI Coastal Union leo wamechapwa 1-0 na Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
  Bao pekee la Polisi Tanzania leo limefungwa na Deusdedit Cossmas dakika ya 52 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 41 baada ya kucheza mechi 30, ingawa wanabaki nafasi ya sita wakizidiwa wastani wa mabao na KMC.
  Coastal Union ambao leo wamepoteza mechi ya tatu mfululizo ya Ligi Kuu na ya nne jumla baada ya kutewa pia kwenye Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wanabaki na pointi zao 33 katika mechi ya 29 sasa katika nafasi ya 13.
  Ikumbukwe timu zitakazoshika nafasi ya 13 na 14 zitakwenda kumenyana na washindi wa pili wa makundi Daraja la Kwanza kuwania kubaki Ligi Kuu, wakati ya 15 hadi 18 zitashuka moja kwa moja.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: COASTAL UNION WAJIWEKA PAGUMU BAADA YA KUCHAPWA MECHI YA TATU MFULULIZO LIGI KUU, TENA MKWAKWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top