• HABARI MPYA

  Friday, May 07, 2021

  NI MAN UNITED NA VILLARREAL FAINALI UEFA EUROPA LEAGUE MEI 26 POLAND

  TIMU ya Manchester United imefanikiwa kwenda fainali ya UEFA Europa League licha ya kuchapwa mabao 3-2 na wenyeji, AS Roma katika mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali usiku wa jana Uwanja wa Olimpico Jijini Roma, Italia.
  Mabao yote ya Manchester United yalifungwa na mshambuliaji mkongwe wa Uruguay, Edinson Cavani dakika ya 39 na 68.
  Na ya Roma yalifungwa na mkongwe wa Bosnia & Herzegovina, Edin Dzeko dakika ya 57, kiungo Mtaliano Bryan Cristante dakika ya 60 na beki Mbrazil, Alex Telles aliyejifunga dakika ya 83.


  Manchester United itakwenda fainali kwa ushindi wa jumla wa 8-5 baada ya kushinda 6-2 kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita England na itutana na Villarreal ya Hispania Mei 26 Uwanja wa Energa Gdansk Jijini Gdansk nchini Poland.
  Villarreal yenyewe imetinga fainali baada ya kuitoa Arsenal kwa mabao 2-1 iliyoshinda Hispania wiki iliyopita kabla ya sare ya 0-0 jana Uwanja wa Emirates.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI MAN UNITED NA VILLARREAL FAINALI UEFA EUROPA LEAGUE MEI 26 POLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top