• HABARI MPYA

  Wednesday, May 12, 2021

  LEICESTER CITY WAIPA UBINGWA MAN CITY BAADA YA KUICHAPA MAN UNITED

   WENYEJI, Manchester United wamechapwa mabao 2-1 na Leicester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Old Trafford.
  Mabao ya Leicester City yamefungwa na Luke Thomas dakika ya 10 na Caglar Soyuncu dakika ya 66, wakati la Manchester United limefungwa na Mason Greenwood dakika ya 15.
  Kwa ushindi huo, Leicester City imefikisha pointi 66 baada ya kucheza mechi 36 na kusogea nafasi ya tatu, wakati Man United inabaki na pointi zake 70 za mechi 35 katika nafasi ya pili, ikiziwa pointi 10 na vinara, Manchester City.


  Matokeo hayo yanamaanisha Man City ni mabingwa wapya wa Ligi Kuu England, kwani pointi zao haziwezi kufikiwa tena na timu nyingine yoyote.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LEICESTER CITY WAIPA UBINGWA MAN CITY BAADA YA KUICHAPA MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top