• HABARI MPYA

  Sunday, May 23, 2021

  AGUERO APIGA MBILI MAN CITY YAICHAPA EVERTON 5-0

  MABINGWA, Manchester City wamekamilisha msimu wa Ligi Kuu ya England kwa ushindi wa 5-0 dhidi ya Everton Uwanja wa Etihad.
  Mabao ya Man City yamefungwa na Kelvin De Bruyne dakika ya 11, Gabriel Jesus dakika ya 14, Phillip Foden dakika ya 53 na Sergio Agüero dakika ya 71 na 76.
  Kwa ushindi huo, Man City imemaliza na pointi 86 mbele ya mahasimu wa Jiji, Manchester United waliomaliza na pointi 74, wakati Everton imemaliza na pointi 59 katika nafasi ya 10 baada ya mechi zote 38 za msimu.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AGUERO APIGA MBILI MAN CITY YAICHAPA EVERTON 5-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top