• HABARI MPYA

  Saturday, May 08, 2021

  SERIKALI YAAMURU MECHI YA SIMBA NA YANGA IANZE SAA 1:00 USIKU BADALA YA 11:00 JIONI LEO UWANJA WA MKAPA

  MCHEZO wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baina watani wa jadi, Simba SC na Yanga SC uliokuwa uanze Saa 11:00 iioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam umesogezwa mbele hadi Saa 1:00 usiku kwa agizo la Serikali.
  Taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) mchana huu imesema kwamba wamepokea agizo la Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuisogeza mbele mechi hiyo hadi Saa 1:00 usiku.
  Mchezo huo marudiano wa msimu baada ya miamba hiyo kutoka sare ya 1-1 kwenye mechi ya kwanza Novemba 7, mwaka jana utaonyeshwa moja kwa moja na chaneli ya AzamSports1HD ya Azam TV.


  Mechi ya kwanza hapo hapo Benjamin Mkapa, Yanga SC walitangulia kwa bao la penalti la mshambuliaji Mghana, Michael Sarpong kipindi cha kwanza, kabla ya beki Mkenya, Joash Onyango kuisawazishia Simba mwishoni kipindi cha pili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SERIKALI YAAMURU MECHI YA SIMBA NA YANGA IANZE SAA 1:00 USIKU BADALA YA 11:00 JIONI LEO UWANJA WA MKAPA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top