• HABARI MPYA

  Sunday, May 16, 2021

  BIASHARA UNITED YALAZIMISHWA SARE YA KUFUNGANA BAO 1-1 NA DODOMA JIJI FC KATIKA LIGI KUU LEO MUSOMA

   WENYEJI Biashara United wamelazimishwa sare ya 1-1 na Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Karume, Musoma mkoani Mara.
  Biashara United walitangulia kwa bao la mapema tu la Lenny David Kisu dakika ya 17, kabla ya Seif Abdallah Karihe kuisawazishia Dodoma Jiji dakika ya 47.
  Kwa matokeo hayo, Biashara United wanafikisha pointi 45 baada ya kucheza mechi 29, ingawa wanabaki nafasi ya nne, wakati Dodoma Jiji sasa wana pointi 39 za mechi 29 katika nafasi ya saba.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BIASHARA UNITED YALAZIMISHWA SARE YA KUFUNGANA BAO 1-1 NA DODOMA JIJI FC KATIKA LIGI KUU LEO MUSOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top