• HABARI MPYA

  Monday, May 10, 2021

  REAL MADRID YALAZIMISHWA SARE YA 2-2 NA SEVILLA NYUMBANI

   TIMU ya Real Madrid imelazimishwa sare ya 2-2 na Sevilla katika mchezo wa La Liga jana Uwanja wa Alfredo Di Stéfano Jijini Madrid na kupoteza nafasi ya kupanda kileleni.
  Sevilla ilitangulia kwa mabao ya Fernando dakika ya 22 na Marco Asensio dakika ya 67 kabla ya Real Madrid kusawazisha kwa mabao ya Ivan Rakitic kwa penalti dakika ya 78 na Eden Hazard dakika ya 90 na ushei.
  Real Madrid inafikisha pointi 75 sawa na Barcelona na inabaki nafasi ya pili, ikizidiwa pointi mbili na Atletico Madrid baada ya wote kucheza mechi 35.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REAL MADRID YALAZIMISHWA SARE YA 2-2 NA SEVILLA NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top