• HABARI MPYA

  Saturday, May 08, 2021

  CHELSEA YAICHAPA MAN CITY 2-1 ETIHAD LIGI KUU ENGLAND

  CHELSEA imeendeleza ubabe kwa Manchester City baada ya kuichapa 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Etihad.
  Manchester City walitangulia kwa bao la Raheem Sterling dakika ya 44, kabla ya Hakim Ziyech kuisawazishia Chelsea dakika ya 63 na Marcos Alonso kufunga la ushindi dakika ya 90 na ushei.
  Kwa ushindi huo, Chelsea inafikisha pointi 64 na kusogea nafasi ya pili, ikiizidi pointi moja Leicester City baada ya wote kucheza mechi 35. 

  Hicho ni kipigo cha pili mfululizo Chelsea inaipa Man City baada ya kuichapa 1-0 katika Nusu Fainali ya Kombe la FA England Aprili 17, bao pekee la Ziyech dakika ya 55 Uwanja wa Wembley, London.
  Timu hizo zitakutana katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Mei 29 Uwanja wa Atatürk Olimpiyat Jijini İstanbul, Uturuki.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA YAICHAPA MAN CITY 2-1 ETIHAD LIGI KUU ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top