• HABARI MPYA

  Saturday, May 15, 2021

  REFA AKATAA BAO LA YACOUBA SOGNE YANGA SC YALAZIMISHWA SARE YA KUFUNGANA NAMUNGO FC RUANGWA

  VIGOGO Yanga SC wamelazimishwa sare ya bila mabao na wenyeji Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
  Hata hivyo mashabiki wa Yanga waliondoka na hasira uwanjani kufuatia refa Hance Mabena wa Tanga kukataa bao lao lililofungwa na mshambuliaji Mburkinabe, Yacouba Sogne kwa kichwa akimalizia mpira wa kona kipindi cha pili.
  Kwa sare hiyo, Yanga SC inafikisha pointi 58 baada ya kucheza mechi 28 na inabaki nafasi ya pili, sasa ikizidiwa pointi tatu na mabingwa watetezi, Simba SC ambao pia wa mechi tatu mkononi, wakati Namungo FC yenyewe inafikisha pointi 36 baada ya mechi 26 nayo pia inabaki nafasi ya 10.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REFA AKATAA BAO LA YACOUBA SOGNE YANGA SC YALAZIMISHWA SARE YA KUFUNGANA NAMUNGO FC RUANGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top