• HABARI MPYA

  Tuesday, May 25, 2021

  KASEKE APIGA ZOTE MBILI YANGA SC YAICHAPA MWADUI FC 2-0 NA KUTINGA NUSU FAINALI AZAM SPORTS FEDERATION CUP

   VIGOGO, Yanga SC wamefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Mwadui FC jioni ya leo Uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.
  Pongezi kwa mfungaji wa mabao yote hayo, kiungo Deus David Kaseke dakika ya 25 na 57 na kwa ushindi huo, Yanga SC watakutana na Biashara United iliyoitoa Namungo FC juzi.
  Robo Fainali za mwisho za michuano hiyo, maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) zitachezwa kesho kati ya Rhino Rangers na Azam FC hapo hapo Kambarage na Simba SC ma Dodoma Jiji FC Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.


  Simba SC ndio mabingwa wa mataji yote kwa sasa nchini, pamoja na ASFC mengine ni ya Ligi Kuu ya Ngao ya Jamii.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KASEKE APIGA ZOTE MBILI YANGA SC YAICHAPA MWADUI FC 2-0 NA KUTINGA NUSU FAINALI AZAM SPORTS FEDERATION CUP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top