• HABARI MPYA

  Sunday, May 30, 2021

  GEITA GOLD NDIYO MABINGWA WA LIGI DARAJA LA KWANZA BAADA YA KUICHAPA MBEYA KWANZA 1-0 LEO UWANJA WA UHURU

   TIMU ya Geita Gold imetwaa ubingwa wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Mbeya Kwanza katika Fainali leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  Katika mchezo huo uliodumu kwa dakika 120 baada ya 90 kumalizika bila timu hizo kufungana, bao pekee la Geita Gold inayofundishwa na kocha mzoefu, Freddy Felix Isaya Kataraiya Minziro 'Majeshi' limefungwa na Omary Ramadhan dakika ya 111.
  Ikumbukwe Mbeya Kwanza na Geita Gold zote zimepanda Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu ujao baada ya kuongoza makundi yao, A na B.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GEITA GOLD NDIYO MABINGWA WA LIGI DARAJA LA KWANZA BAADA YA KUICHAPA MBEYA KWANZA 1-0 LEO UWANJA WA UHURU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top