• HABARI MPYA

  Sunday, May 23, 2021

  ROBERT LEWANDOWSKI AVUNJA REKODI YA GERD MULLER BUNDESLIGA

   MSHAMBULIAJI Robert Lewandowski jana amefikisha mabao 41 msimu huu, Bayern Munich ikiichapa Augsburg 5-2 na kuvunja rekodi ya mabao mengi msimu mmoja katika iliyowekwa na gwiji wa Bayern, Gerd Muller msimu wa 1971-72 kwa mabao yake 40.
  Lewandowski alifunga bao lake la 41 dakika ya 90, hiyo ikiwa ni mechi ya 10 mfululizo anafunga na kwa ujumla amefunga mabao yote hayo katika mechi 29 msimu huu, Bayern ikitwaa taji la tisa mfululizo na la rekodi baada ya kumaliza na pointi 78 – 13 zaidi ya RB Leipzig waliomaliza nafasi ya pili.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ROBERT LEWANDOWSKI AVUNJA REKODI YA GERD MULLER BUNDESLIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top