• HABARI MPYA

  Wednesday, May 26, 2021

  NAMUNGO FC YAICHIMBIA KABURI GWAMBINA FC BAADA YA KUICHAPA 1-0 LEO RUANGWA BAO PEKEE LA LUSAJO

   BAO la dakika ya 90 na ushei la mshambuliaji Relliant Lusajo limetosha kuipa Namungo FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Gwambina FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
  Kwa ushindi huo, Namungo FC imefikisha pointi 40 baada ya kucheza mechi 28 na kusogea nafasi ya nane kutoka ya 10.
  Gwambina FC inabaki na pointi zake 31 za mechi 30 sasa katika nafasi ya 17 kwenye ligi ya timu 18, ambayo mwisho wa msimu tatu zitashuka na mbili zitakwenda kucheza na timu za Daraja la Kwanza kuwania kubaki Ligi Kuu.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NAMUNGO FC YAICHIMBIA KABURI GWAMBINA FC BAADA YA KUICHAPA 1-0 LEO RUANGWA BAO PEKEE LA LUSAJO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top