• HABARI MPYA

  Wednesday, May 26, 2021

  AZAM FC YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA TFF BAADA YA KUITANDIKA RHINO RANGERS 3-1 LEO UWANJA WA KAMBARAGE MJINI SHINYANGA

   TIMU ya Azam FC imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora jioni ya leo Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
  Mabao ya Azam FC na sasa wanasubiri mshindi kati ya Simba vs Dodoma Jiji, itakayoanza saa 1:00 usiku wa leo. 
  Ayoub Lyanga dakika ya 34, Agrey Morris kwa penalti dakika ya 65 na Mzambia Obrey Chirwa dakika ya 81, wakati la Rhino limefungwa na Selemani Abdallah dakika ya 32.


  Sasa Azam FC inasubiri mshindi wa mchezo kati ya mabingwa watetezi, Simba SC na Dodoma Jiji FC zinazomenyana usiku wa leo Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam ikutane katika Nusu Fainali Uwanja wa Maji Maji mjini Songea mwezi ujao.
  Nusu Fainali nyingine ni kati ya Biashara United ya Mara na Yanga SC ya Dar es Salaam itakayopigwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA TFF BAADA YA KUITANDIKA RHINO RANGERS 3-1 LEO UWANJA WA KAMBARAGE MJINI SHINYANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top