• HABARI MPYA

  Thursday, May 27, 2021

  KAMATI YA UTENDAJI YAKUTANA LEO DAR NA KUAMUA UCHAGUZI MKUU WA TFF UFANYIKE AGOSTI 7, MWAKA HUU

   UCHAGUZI Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) utafanyika Agosti 7, mwaka huu, imeelezwa.
  Hayo yamesemwa na Rais wa TFF, Wallace Karia katika taarifa yake kwa vyombo vya Habari kufuatia kikao cha Kamati ya Utendaji ya shirikisho hilo kilichofanyika leo ambacho ni cha kawaida cha kikatiba kuzungumzia ajenda za maendeleo ya soka.
  "Tumepitisha tarehe ya mkutano Mkuu wa TFF kwamba itakuwa ni tarehe 7 Agosti na tarehe hiyo tutampelekea pia Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi kumuambia kwamba ni tarehe ambazo tumezipanga kwa mkutano wetu, kwa hiyo na yeye ataendelea kwa taratibu zake, kwa sababu kwenye ajenda yetu, ajenda za Mkutano Mkuu mojawapo inakuwa ni uchaguzi," amesema Karia.

  Aidha, Karia amesema kwamba katika kikao cha Kamati ya Utendaji wamepokea taarifa ya utekelezaji na kuzungumzia miradi ya ujenzi wa vituo vya Kigamboni Jijini Dar es Salaam na Mnyanjani, Tanga.
  "Lakini pia tumekuwa na kupokea taarifa kutoka Kamati yetu ya Sheria kwenye marekebisho ya baadhi ya kanuni za uendeshaji zinazosimamia Kamati zetu mbalimbali, ikiwemo Kamati zetu za Ukaguzi pamoja na kupitisha makabrasha ambayo yatatumika kuendesha hizo za Kamati zetu," ameongeza Karia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAMATI YA UTENDAJI YAKUTANA LEO DAR NA KUAMUA UCHAGUZI MKUU WA TFF UFANYIKE AGOSTI 7, MWAKA HUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top