• HABARI MPYA

  Wednesday, May 12, 2021

  NAMUNGO FC YAWACHIMBIA KABURI MTIBWA SUGAR BAADA YA KUWACHAPA 1-0 LEO RUANGWA

   TIMU ya Namungo FC imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
  Bao pekee la Namungo FC leo limefungwa na Ibrahim Abdallah dakika ya 19 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 35 baada ya kucheza mechi 25 na kusogea nafasi ya 10.
  Hali ni mbaya kwa Mtibwa Sugar, mabingwa wa 1999 na 2000 baada ya kipigo cha leo wanabaki na pointi zao 28 za mechi 28 katika nafasi ya 17 kwenye ligi ya timu 18.


  Timu nne zitashuka daraja mwishoni mwa msimu, wakati mbili zitakwenda kucheza na timu za Daraja la Kwanza kuwania kubaki Ligi Kuu.
  Mechi nyingine ya Ligi Kuu, Ihefu SC imelazimishwa sare ya 1-1 na Polisi Tanzania Uwanja wa Highland Estate, Ubaruku mkoani Mbeya.
  Ihefu SC inafikisha pointi 31 baada ya mechi 29 katika nafasi ya 12, wakati Polisi Tanzania sasa wana pointi 38 za mechi 29 katika nafasi ya sita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NAMUNGO FC YAWACHIMBIA KABURI MTIBWA SUGAR BAADA YA KUWACHAPA 1-0 LEO RUANGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top