• HABARI MPYA

  Tuesday, May 11, 2021

  SIMBA SC NA DODOMA JIJI DAR, YANGA SC NA MWADUI SHINYANGA ROBO FAINALI AZAM SPORTS FEDERATION CUP

  MABINGWA watetezi, Simba watamenyana na Dodoma Jiji FC katika Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup mwishoni mwa mwezi huu.
  Wapinzani wao wa jadi, Yanga SC wao watatoka tena kuifuata Mwadui FC huko Shinyanga, wakati Azam FC watakuwa wageni wa Rhino Rangers ya Tabora na Biashara United itakutana na Namungo FC.
  Mechi zote za Robo Fainali ya ASFC zitachezwa kati ya Mei 24 na 26, mwaka huu na kuonyeshwa LIVE na Azam Sports.

  Mshindi kati ya Mwadui FC na Yanga SC atakutana na mshindi kati ya Biashara United na Namungo FC na mshindi kati ya Simba na Dodoma Jiji atakutana na mshindi kati ya Rhino Rangers Azam FC katika Nusu Fainali.
  Nusu Fainali zitachezwa kati ya mwishoni mwa Juni na mwanzoni mwa Julai, wakati Fainali itafanyika katikati ya Julai Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC NA DODOMA JIJI DAR, YANGA SC NA MWADUI SHINYANGA ROBO FAINALI AZAM SPORTS FEDERATION CUP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top