• HABARI MPYA

    Sunday, May 30, 2021

    CHELSEA BINGWA ULAYA, YAIPIGA MAN CITY 1-0 URENO

    TIMU ya Chelsea imefanikiwa kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Manchester City usiku huu Uwanja wa Do Dragão Jijini Porto, Ureno.
    Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee Mjerumani, Kai Havertz dakika ya 42 akimalizia pasi ya kiungo mwingine wa kimataifa wa England, Mason Mount.
    Hilo linakuwa taji la pili tu la Ligi ya Mabingwa kwa The Blues baada ya lile walilolitwaa msimu wa 2011–2012 wakiwafunga wenyeji, Bayern Munich katika fainali Uwanja wa Allianz Arena Jijini Munich, Ujerumani kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya 1-1 chini ya kocha wa muda, Mtaliano Roberto Di Matteo.


    Ushindi huu ni mwendelezo wa ubabe wa kocha Mjerumani, Thomas Tuchel kwa kocha Mspaniola wa mabingwa wa Ligi Kuu ya England, Pep Guardiola baada ya kuifunga pia Man City 1-0 kwenye Nusu Fainali ya Kombe la FA Aprili 17 na 2-1 kwenye ligi Mei 8.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHELSEA BINGWA ULAYA, YAIPIGA MAN CITY 1-0 URENO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top