• HABARI MPYA

  Sunday, May 30, 2021

  PAMBA SC NA TRANSIT CAMP ZAPANGIWA WAPINZANI VITA YA KUWANIA KUPANDA LIGI KUU MSIMU UJAO

  MABINGWA wa zamani wa Ligi Kuu ya Muungano, Pamba FC ya Mwanza itamenyana na timu itakayomaliza nafasi ya 13 kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu kuwania kupanda ligi hiyo msimu ujao.
  Katika droo iliyochezeshwa leo Dar es Salaam, Transit Camp itamenyana na timu itakayomaliza nafasi ya 14 kwenye Ligi Kuu msimu huu.
  Mechi za kwanza zitachezwa Julai 21 na timu za Daraja la Kwanza zote zitaanzia nyumbani kabla ya kusafiri kuzifuata timu za Ligi Kuu kwa mechi za marudiano Julai 24.


  Mbeya Kwanza na Geita Gold zimepanda moja kwa moja baada ya kuongoza makundi A na B, wakati Transit Camp na Pamba zinapitia kwenye mchujo, maarufu kama Play-Offs kuwania kupanda.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PAMBA SC NA TRANSIT CAMP ZAPANGIWA WAPINZANI VITA YA KUWANIA KUPANDA LIGI KUU MSIMU UJAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top