• HABARI MPYA

  Sunday, May 23, 2021

  ASTON VILLA YAWACHAPA CHELSEA 2-1 VILLA PARK

  TIMU ya Chelsea imekamilisha msimu wa Ligi Kuu ya England kwa kuchapwa 2-1 na wenyeji, Aston Villa Uwanja wa Villa Park Jijini Birmingham.
  Mabao ya Aston Villa yamefungwa na Bertrand Traoré dakika ya 43 na Anwar El Ghazi kwa penalti dakika ya 52, wakati la Chelsea limefungwa na Ben Chilwell dakika ya 70.
  The Blues inabaki na pointi zake 67 ikishukia nafasi ya nne, nyuma ya Liverpool yenye pointi 69, wakati Aston Villa inamaliza na pointi zake 55 katika nafasi ya 11 baada ya mechi zote 38 za msimu.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ASTON VILLA YAWACHAPA CHELSEA 2-1 VILLA PARK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top