• HABARI MPYA

  Saturday, May 29, 2021

  PAMBA YABISHA HODI LIGI KUU BAADA YA KUITANDIKA KEN GOLD 4-1 LEO UWANJA NYAMAGANA JIJINI MWANZA

   MABINGWA wa zamani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pamba SC wamefanikiwa kufuzu hatua ya kuwania kupanda Ligi Kuu msimu ujao baada ya ushindi wa 4-1 dhidi ya Ken Gold leo Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.
  Pamba wanasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-3 kufuatia kufungwa 2-0 kwenye mchezo wa kwanza.
  Nayo Transit Camp ya Dar es Salaam imefanikiwa kuwatoa mabingwa wengine wa zamani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, African Sports kwa penalti 5-4 kufuatia sare ya jumla ya 1-1 kila timu ikishinda 1-0 nyumbani, mechi ya marudiano ikichezwa leo Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.


  Sasa Pamba na Transit Camp iliyowahi kucheza Ligi Kuu pia zitamenyana na timu zitakazoshika nafasi ya 13 na 14 Ligi Kuu msimu huu kuwania kupanda.
  Droo ya mechi hizo itafanyika kesho Dar es Salaam na timu hizo zitacheza mechi mbili nyumbani na ugenini na washindi wa jumla watapanda, au kubaki Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PAMBA YABISHA HODI LIGI KUU BAADA YA KUITANDIKA KEN GOLD 4-1 LEO UWANJA NYAMAGANA JIJINI MWANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top