• HABARI MPYA

  Tuesday, May 11, 2021

  KAGERA SUGAR YAICHAPA MWADUI FC 3-0 KISHAPU NA KUJIONDOA ENEO LA HATARI ZAIDI LIGI KUU

  TIMU ya Kagera Sugar imewachapa wenyeji, Mwadui FC 3-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Mwadui Complex, Kishapu mkoani Shinyanga.
  Mabao ya Kagera Sugar yamefungwa na David Luhende dakika ya 45 na ushei, Yussuf Mhilu dakika ya 68 na Erick Mwijage dakika ya 90 na ushei.
  Kwa ushindi huo, Kagera Sugar inafikisha pointi 30 baada ya kucheza mechi 29 na kusogea nafasi ya 13 kutoka ya 17, wakati Mwadui FC inaendelea kushika mkia na pointi zake 19 za mechi 29.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAGERA SUGAR YAICHAPA MWADUI FC 3-0 KISHAPU NA KUJIONDOA ENEO LA HATARI ZAIDI LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top