• HABARI MPYA

  Wednesday, May 26, 2021

  BOCCO APIGA MBILI SIMBA SC YAICHAPA DODOMA JIJI 3-0 NA KUTINGA NUSU FAINALI KOMBE LA TFF, ITAKUTANA NA AZAM SONGEA

   MABINGWA watetezi, Simba SC wamefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Simba SC leo yamefungwa na Nahodha John Raphael Bocco, la kwanza kwa penalti dakika ya 23 na lingine dakika ya 42 wakati la tatu limefungwa na mshambuliaji mwenzake, Mnyarwanda mwenye asili ya Uganda, Meddie Kagere dakika ya 79.
  Sasa Simba SC itakutana ma Azam FC iliyoitoa Rhino Rangers ya Tabora leo pia kwa kuichapa mabao 3-1 Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.


  Mechi hiyo itachezwa Uwanja wa Maji Maji mjini Songea, wakati Nusu Fainali nyingine itazikutanisha Biashara United na Yanga SC Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora mwezi ujao.
  Biashara United waliitoa Namungo FC Jumapili Uwanja wa Karume, Musoma mkoani Mara na Yanga wameitoa Mwadui jana FC Uwanja wa Kambarage, Shinyanga wote kwa ushindi wa mabao 2-0.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BOCCO APIGA MBILI SIMBA SC YAICHAPA DODOMA JIJI 3-0 NA KUTINGA NUSU FAINALI KOMBE LA TFF, ITAKUTANA NA AZAM SONGEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top