• HABARI MPYA

  Thursday, May 20, 2021

  PEPE APIGA MBILI ARSENAL YAICHAPA CRYSTAL PALACE 3-1

   TIMU ya Arsenal imeibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya wenyeji, Crystal Palace katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa jana Uwanja wa Selhurst Park Jijini London.
  Mabao ya Arsenal yamefungwa na Nicolas Pépé dakika ya 35 na 90 na ushei na Martinelli dakika ya 90, wakati la Crystal Palace limefungwa na Christian Benteke dakika ya 62.
  Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 58 baada ya kucheza mechi 37 na kusogea nafasi ya tisa, wakati Crystal Palace inabaki na pointi zake 44 za mechi 37 katika nafasi ya 13.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PEPE APIGA MBILI ARSENAL YAICHAPA CRYSTAL PALACE 3-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top